Tuesday, January 23, 2024

HOLY MASS READINGS FOR WEDNESDAY, JANUARY 24, 2024 (SWAHILI)

MASOMO YA IBADA YA MISA YA KILA SIKU

JUMATANO, JUMA LA TATU KATIKA KIPINDI CHA KAWAIDA.

KUMBUKUMBU: Mt. Fransisko wa Sale, Askofu na Mwalimu wa Kanisa

Zaburi: Juma la Tatu

SOMO LA KWANZA
"Nitamwinua mzao wako baada yako, nami nitaujenga ufalme wake. "
Somo katika kitabu cha pili cha Samueli 7:4-17

Siku zile:
Neno la Bwana lilimjia Nathani kusema: Nenda ukamwambie
mtumishi wangu Daudi, Bwana anasema hivi: Je, wewe utanijengea
nyumba, nikae ndani yake? Mimi sijakaa katika nyumba tangu
siku ile niliyowatoa Waisraeli kutoka Misri, hata leo, lakini
nimezunguka katika hema na kibanda. Wakati wote nimesafiri
na Waisraeli, nimewahi kumwambia mmoja wa waamuzi wa
Israeli niliowaweka kuwaongoza watu wangu Israeli, nikisema:
Mbona hamkunijengea nyumba ya mierezi?
Sasa ukamwambie mtumishi wangu Daudi ifuatavyo:
Bwana wa majeshi asema hivi: Mimi nalikutwaa katika kazi ya
kuwalisha na kuwaandama kondoo ili uwe mkuu juu ya watu
wangu Israeli, nimekuwa pamoja nawe popote ulipokwenda na
nimewaondosha maadui zako wote mbele yako. Nami nitakufanyia
jina kuu, kama jina la wakuu waliopo duniani. Nami nitawawekea
mahali watu wangu Israeli, nitawapanda wapate kukaa mahali
pao wenyewe, wasiweze kuondolewa tena, wala wana wa uovu
hawatawasumbua tena, kama hapo zamani, tangu nilipowaweka
waamuzi juu ya Israeli watu wangu. Nami nitakustarehesha mbele
ya adui zako wote. Tena, Bwana anakufunulia kuwa atakujengea
nyumba. Na siku zako zitakapotimia, nawe umejipumzisha na baba
zako, nitamwinua mzao wako, baada yako atokaye viunoni mwako,
nami nitauimarisha ufalme wake. Yeye ndiye atakayenijengea
nyumba kwa jina langu, nami nitakiimarisha kiti chake cha enzi
daima. Mimi nitakuwa baba yake, naye atakuwa mwanangu; na
akitenda uovu nitamwadhibu kwa fimbo watumiayo watu na
mapigo wapigayo wanadamu. Bali sitamwondolea fadhili zangu,
kama nilivyomwondolea mtangulizi wako, Sauli, ambaye
nilimwondoa mbele yangu. Nayo nyumba yako na ufalme wako
vitadumu milele mbele yangu, na kiti chako kitakaa imara milele."
Nathani aliyanena maneno hayo na ufunuo huo wote kwa Daudi.

Neno la Bwana.

ZABURI YA KUITIKIZANA
Zaburi 89:4-5, 27-28, 29-30 (K. 29a)

K. Nitadumisha fadhili zangu hata milele.

"Nimefunga agano na mteule wangu;
nimemwapia Daudi, mtumishi wangu:
nitawasimika wazao wako hata milele,
nitaimarisha kiti cha ufalme wako kwa vizazi vyote. K.

Yeye ataniita, Wewe ni Baba yangu,
Mungu wangu na mwamba wa wokovu wangu.
Nami nitamweka awe mzaliwa wangu wa kwanza,
kuwa juu sana kuliko wafalme wa dunia, K.

Nitamhifadhia fadhili zangu hata milele:
na agano langu kwake litadumu kuwa imara.
Nitasimika uzazi wake milele.
na kiti chake cha enzi kitadumu kama mbingu." K.

SHANGILIO LA INJILI

Aleluya.

Mbegu ni neno la Mungu, anayepanda ni Kristo; atakayempata ataishi milele.

Aleluya.

INJILI
"Mpanzi alikwenda shambani kupanda mbegu."
Somo a Injili takatifu ilivyoandikwa na Marko 4:1-20

Wakati ule: Yesu alianza kufundisha tena kando ya ziwa. Kundi
kubwa lilikusanyika mbele yake, hata akaingia katika chombo ziwani
akaketi humo. Watu wote walikaa kando ya ziwa. Aliwafundisha
mengi kwa mifano, na katika mafundisho yake aliwaambia.
"Sikilizeni! Mpanzi alikwenda shambani kupanda mbegu. Katika
kupanda, mbegu nyingine zilianguka kando ya njia, wakaja ndege.
wakazidonoa. Nyingine zilianguka penye changarawe pasipo
udongo mwingi. Zikaota upesi lakini chini kina hakikupatikana,
Na jua lilipochomoza ziliungua, zikanyauka kwa kukosa mizizi.
Nyingine zilianguka kati ya miiba na miiba ikamea, ikazisonga,
zisitoe mavuno. Nyingine zilianguka katika udongo mzuri, zikaota,
zikakua, zikazaa moja thelathini, nyingine sitini, na nyingine
mia." Akasema, "Aliye na masikio ya kusikilizia, na asikie."
Baadaye alipokuwa peke yake, wale Kumi na Wawili pamoja
na wafuasi wake walimwuliza maana ya mifano. Akawajibu,
*Ninyi mmejaliwa kujua mfano wa ufalme wa Mungu, bali wale
walio nje hupewa yote kwa mifano, ili 'kuona waone, wasitambue,
kusikia wasikie, wasielewe, wasije wakaongoka na dhambi
kusamehewa. "
Yesu akawaambia,
"Je, hamwelewi mfano huu? Mtawezaje kufahamu mifano yoyote?
Mpanzi analipanda neno. Hawa ni wale walio kando ya njia
wakati neno linapopandwa. Mara wanapolisikia, Shetani huja,
akalichukua neno lililopandwa mioyoni mwao. Na wale waliopandwa kwenye changarawe ni wale ambao,wanapolisikia neno, mara wanalipokea kwa furaha. Ila hawana
mizizi ndani mwao; wanalipokea kwa muda tu. Panapotokea
matatizo au madhulumu kwa ajili ya hilo neno, mara wanakwazwa.
Wale waliopandwa kati ya miiba, hao ni wale wanaolisikia neno,
lakini shughuli za dunia, na ulaghai wa mali, na tamaa za mambo
mengine zinaingia kulisonga neno, na hivyo neno halizai kitu.Kisha waliopandwa katika udongo wenye rutuba,hawa ndio wanaolisikia neno, wakalipokea,
wakazaa matunda mmoja thelathini, mmoja sitini, na mmoja mia."

Injili ya Bwana.

No comments:

Post a Comment