MASOMO YA IBADA YA MISA YA KILA SIKU
JUMANNE, JUMA LA TATU KATIKA KIPINDI CHA KAWAIDA.
Zaburi: Juma la Tatu
SOMO LA KWANZA
"Daudi na taifa lote la Israeli wakalipeleka sanduku
la Bwana kwa shangwe."
Somo katika kitabu cha pili cha Samueli 6:12b-15, 17-19
"Daudi na taifa lote la Israeli wakalipeleka sanduku
la Bwana kwa shangwe."
Somo katika kitabu cha pili cha Samueli 6:12b-15, 17-19
Siku zile:
Daudi alienda, akalipandisha sanduku la Mungu kutoka nyumba
ya Obed-edomu hadi katika mji wa Daudi kwa shangwe. Ikawa
watu waliolichukua sanduku la Bwana walipopiga hatua sita
Daudi akachinja ng'ombe na kondoo mnono kuwa sadaka.
Akiwa amevaa naivera ya kitani, Daudi alicheza mbele ya Bwana,
kwa nguvu zake zote. Daudi na taifa lote la Israeli wakalipandisha
sanduku la Bwana kwa shangwe na sauti ya baragumu.
Wakaliingiza sanduku la Bwana na kuliweka mahali pake, katikati
ya hema aliyopiga Daudi kwa ajili yake, naye Daudi akatolea sadaka
za kuteketezwa na sadaka za amani mbele ya Bwana.
Alipomaliza kutolea sadaka hizo mbele ya Bwana wa majeshi,
Daudi akawabariki watu kwa jina la Bwana wa majeshi. Kisha
akawagawia watu wote wa Israeli, waume kwa wake kila mtu
mkate wa ngano, na kipande cha nyama, na mkate wa zabibu kavu.
Halafu watu wote wakaenda zao, kila mtu nyumbani kwake.
Neno la Bwana.
ZABURI YA KUITIKIZANA
Zaburi 24:7, 8,9, 10 (K. 8a)
K. Ni nani mfalme wa utukufu? Ndiye Bwana!
Inueni vichwa vyenu, enyi malango;
inukeni, enyi malango ya kale.
Na aingie mfalme wa utukufu! K.
Ni nani huyu mfalme wa utukufu?
Ndiye Bwana mwenye nguvu na enzi;
Bwana, hodari wa vita. K.
Inueni vichwa vyenu, enyi malango;
inukeni, enyi malango ya kale.
Mfalme wa utukufu na apate kuingia! K.
Ni nani huyu mfalme wa utukufu?
Ndiye, Bwana wa majeshi,
ndiye mfalme wa utukufu.K.
SHANGILIO LA INJILI
Mathayo 11:25
Aleluya.
Utukuzwe, Baba, Bwana wa mbingu na dunia,
kwa kuwa umewafunulia watoto wachanga mafumbo ya ufalme.
Aleluya.
INJILI
"Kila ayafamyaye mapenzi ya Mungu,
huyo ndiye ndugu yangu, na dada yangu, na mama yangu."
Somo la Injili takatifu ilivyoandikwa na Marko 3:31-35
Wakati ule:
Mama na ndugu zake Yesu walifika. Nao wakisimama nje, walituma
habari kwake, kwa maana alizungukwa na watu wengi. Basi
wakamwambia, "Tazama, mama yako na ndugu zako wapo nje,
wanakutafuta."
Lakini aliwajibu, "Mama yangu na ndugu zangu ni akina nani?"
Akawatazama wale waliomzunguka, akasema,
"Hawa ni mama yangu na ndugu zangu. Kwa maana kila afanyaye
mapenzi ya Mungu, huyo ndiye kaka yangu, na dada yangu, na mama
yangu."
Injili ya Bwana.
No comments:
Post a Comment