Translate

Sunday, January 21, 2024

HOLY MASS READINGS FOR MONDAY, JANUARY 22, 2024 (SWAHILI)

JUMATATU, JUMA LA TATU KATIKA KIPINDI CHA KAWAIDA.

Zaburi Juma la Tatu


SOMO LA KWANZA
"Wewe utawalisha watu wangu Israeli.
Somo katika kitabu cha pili cha Samueli 5:1-7, 10

Wakati ule: Makabila yote ya Israeli yalimwendea Daudi huko
Hebroni na kusema, "Tazama, sisi hapa ni mfupa wako, na
nyama yako. Hapo zamani Sauli alipokuwa nfalme wetu, wewe
uliwaongoza Waisraeli kuingia na kutoka vitani. Na Bwana
akakuambia: Wewe utawalisha watu wangu Israeli, nawe utakuwa
mkuu juu ya Israeli." 
Basi, wazee wote wa Israeli wakamwendea mfalme huko Hebroni,
naye mfalme Daudi akafanya nao mapatano huko Hebroni mbele ya
Bwana, wakampaka mafuta awe mfalme wa Israeli. Daudi alikuwa
na miaka thelathini alipoanza kutawala, na alitawala kwa miaka
arobaini: yaani miaka saba na miezi sita huko Hebroni juu ya
Yuda, na kule Yerusalemu alitawala miaka thelathini na mitatu juu
ya Israeli yote na Yuda. Kisha mfalme na watuwake wakaelekea
Yerusalemu ili kupigana na Wayebusi waliokalia nchi ile.
Daudi akaambiwa na wenyeji hao, “Huwezi kuingia humu; vipofu na
viwete watakufukuza!" Ikiwa ni mbinu yao ya kumwambia Daudi:
kuwa hawezi kuingia humo. Lakini Daudi, aliipiga ngome ya Sioni
akaitwaa, ukawa ndio mji wa Daudi. Daudi akazidi kuimarika
na kustawi, kwa maana Bwana wa majeshi alikuwa pamoja naye.

Neno la Bwana.

ZABURI YA KUITIKIZANA
Zaburi 89:20, 21-22, 25-26 (K. 25a)

K. Uaminifu wangu na fadhili zangu zitakuwa naye.

Awali uliwaambia waaminifu wako katika maono, ukasema:
"Nimempa aliye hodari msaada,
nimemkuza kijana kutoka miongoni mwa watu. K.

Nimemchagua Daudi, mtumishi wangu;
nimempaka mafuta yangu matakatifu.
Mkono wangu utakuwa tegemeo lake;
mkono wangu utamtia nguvu. K.

Uaminifu wangu na fadhili zangu zitakuwa naye;
na kwa jina langu pembe yake itatukuka.
Nitanyosha mkono wake juu ya bahari,
na mkono wake wa kulia juu ya mito." K.

SHANGILIO LA INJILI
2 Timotheo 1:10

Aleluya.

Mwokozi wetu Kristo Yesu ameyashinda mauti
na akaleta uzima wa milele kwa njia ya Injili.

Aleluya.

INJILI
"Shetani anafikia mwisho wake"
Somo la Injili takatifu ilivyoandikwa na Marko 3:22-30

Wakati ule: Waandishi waliokuja kutoka Yerusalemu walisema,
Amepagawa na Beelzebuli, na kwa msaada wa mkuu wa pepo wabaya huwatoa pepo wabaya." 
[Yesu] akawaita na kuanza
kuwaambia kwa mifano, "Awezaje Shetani kumtoa ShetanĂ­? Ufalme
wawezaje kusimama ukiwa umegawanyika wenyewe? Kadhalika
nyumba ikiwa imegawanyika yenyewe, nyumba hiyo haiwezi
kusimama.
Na kama Shetani akijipinga mwenyewe na kugawanyika, hawezi
kusimama, bali amefika mwishoni. Hakuna awezaye kuingia
katika nyumba ya mwenye nguvu na kupokonya vitu vyake,
isipokuwa amemfunga kwanza yule mwenye nguvu. Hapo
tu aweza kupokonya vitu nyumbani mwake.
Amin, nawaambieni, wanadamu huondolewa dhambi zote
na kufuru zao. Lakini mtu anayemkufuru Roho Mtakatifu,
hana maondoleo hata milele, bali atastahili hukumu ya milele."
Alisema hayo kwa sababu walisema, "Ana pepo mchafu."

Injili ya Bwana.

No comments:

Post a Comment

HOLY MASS READINGS FOR NOVEMBER 15, 2024

Friday of  the Thirty Second Week in Ordinary Weekday  (White) Memorial of St. Albert the Great, Bishop and Doctor LH: Office of  Memorial, ...