Translate

Thursday, January 25, 2024

HOLY MASS READINGS FOR FRIDAY, JANUARY 26, 2024 (SWAHILI)

MASOMO YA IBADA YA MISA YA KILA SIKU

IJUMAA, JUMA LA TATU KATIKA KIPINDI CHA KAWAIDA.

Kumbukumbu: Wat. Timotheo na Tito, Maaskofu

Misa ya wachungaji

Zaburi: Sala ya Siku 

SOMO LA KWANZA
"Hayo yanikumbusha imani yako isiyo na unafiki."
Somo katika barua ya pili ya Mtakatifu Paulo kwa Timotheo 1:1-8

Mimi Paulo, kwa kusudio la Mungu mtume wa Kristo Yesu, kadiri
ya ahadi ya uzima unaopatikana katika Kristo Yesu, nakusalimu
wewe, Timotheo, mwanangu mpendwa: neema, huruma na amani zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu, Bwana wetu, ziwe
nawe. Namshukuru Mungu, ambaye namtumikia kwa dhamiri safi
kutokana na wazee wangu. Nawe ninakukumbuka daima katika sala
zangu usiku na mchana. Nikikumbuka machozi yako ninatamani
kukuona nipate kujazwa tena furaha. Hayo yanikumbusha
imani yako isiyo na unafiki iliyokaa kwanza katika bibi yako
mzee Loisi na mama yako Eunike na, nina hakika, ndani yako pia.
Ninakukumbusha, uiamshe neema ya Mungu iliyomo ndani yako
kwa kuwekewa mikono yangu. Kwa maana Mungu hakutupelekea
roho ya woga, bali Roho wa nguvu na wa upendo na wa kushika kiasi.
Basi, usione aibu kumshuhudia Bwana wetu, wala usione aibu kwa
sababu yangu mimi niliye mfungwa wake. Bali uvumilie pamoja nami
kwa ajili ya Injili ukitegemea nguvu ya Mungu.

Neno la Bwana.

AU SOMO LIFUATALO:

SOMO LA KWANZA

"Tito, mwanangu wa kweli kadiri ya imani moja tunayoishiriki."
Somo katika barua ya Mtakatifu Paulo kwa Tito 1:1-5

Mimi Paulo, mtumishi wa Mungu na mtume wa Yesu Kristo, nimeitwa
kuwapatia wateule wa Mungu imani na ujuzi wa uchaji wa kweli
nikitazamia uzima wa milele, ambao Mungu asiyepitiwa ameuahidi
kabla ya nyakati zote. wakati wake, amefafanua neno lake katika tangazo
Lakini sasa, nililokabidhiwa mimi kwa agizo la Mungu, Mwokozi wetu. Salamu
kwako Tito, mwanangu wa kweli kadiri ya imani moja tunayoishiriki.
Neema na amani zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu, Mwokozi wetu, ziwe nawe.
Nimekuacha huko Krete kusudi uratibishe yasiyopangwa bado, na
uweke wazee wa Kanisa katika kila mji kama nilivyokuagizia.

Neno la Bwana.

ZABURI YA KUITIKIZANA
Zaburi 96: 1-2a, 2b-3, 7-8a, 10 (K. 3)

K. Yahubirini maajabu ya Bwana kati ya watu wote.

Mwimbieni Bwana wimbo mpya;
mwimbieni Bwana, nchi yote.
Mwimbieni Bwana, lisifuni jina lake. K.

Siku kwa siku tangazeni wokovu wake.
Uhubirini utukufu wake kati ya mataifa,
maajabu yake, kati ya watu wote. K.

Mpeni Bwana, enyi jamaa za mataifa,
mpeni Bwana sifa na enzi:
mpeni Bwana utukufu wa jina lake! K.

Waambieni mataifa: Bwana ni mfalme.
Amekaza ulimwengu usitikisike,
atawahukumu watu kwa haki. K.

SHANGILIO LA INJILI
Luka 4:18

Aleluya.

Bwana amenituma niwahubirie maskini habari njema,
kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao.

Aleluya.

INJILI
"Mavuno ni mengi, lakini wafanyakazi ni wachache."
Somo la Injili takatifu ilivyoandikwa na Luka 10:1-9

Wakati ule: Bwana aliweka wengine sabini na wawili, aliowatuma
wawili wawili wamtangulie katika miji na vijiji vyote alivyotaka
kuvitembelea mwenyewe.
Akawaambia, "Mavuno ni mengi, lakini wafanyakazi ni wachache;
basi, mwombeni Bwana wa mavuno, apeleke wafanyakazi katika
mavuno yake. Nendeni; angalieni, nawatuma kama wanakondoo
kati ya mbwamwitu. Msichukue mfuko wa fedha, wala mkoba,
wala viatu, wala msimsalimie mtu njiani.
Kila nyumba mnayoingia, semeni kwanza, Amani iwe na
nyumba hii. Na ikiwa mwana wa amani yumo, amani yenu itatua
juu yake; lakini ikiwa hayumo, amani yenu itarudi kwenu. Kaeni
katika nyumba hiyo mkila na kunywa mpewavyo nao, maana
mfanyakazi astahili mshahara wake. Msiende toka nyumba hata
nyumba. Mkiingia mjini wanapowapokea, mle mnachoandaliwa,
waponyeni wagonjwa waliopo, mkawaambie watu, Ufalme wa
Mungu umewakaribia."

Injili ya Bwana.


No comments:

Post a Comment

HOLY MASS READINGS FOR DECEMBER 21, 2024

Saturday of  the Third Week of Advent, Year C  (Purple) LH: Office of the Day, Week III Mass of the day, Preface II of Advent FIRST READING ...